May 18, 2017



Kikosi cha Yanga kinarejea uwanjani leo kuanza maandalizi ya mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu Bara.

Wachezaj hao watarejea mazoezini leo na kuanza kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa, hii ikiwa ni baada ya mapumziko ya siku moja.

Wachezaji wa Yanga walipewa mapumziko ya siku moja ikiwa ni baada ya kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Toto African.
Yanga iko kileleni mwa ligi ikiwa imejihakikishia ubingwa huku Simba wakiamini watafanya miujiza.


Miujiza wanayosubiri Simba ni kushinda mechi ya mwisho kwa zaidi ya mabao matano dhidi ya Mwadui FC na Yanga wafungwe na Mbao FC ikiwezekana zaidi ya mabao matatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic