Simba wanaamini bado wana nafasi ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara licha ya kuonekana kama nguvu yao imepoteza mwelekeo.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja amesema wanachotaka wao ni kuendelea kupambana na kushinda mechi zao mbili zilizobaki.
“Hatuwezi kukata tamaa, kuna mechi mbili na tunataka kupata pointi sita, baada ya hapo mengine yatafuatia au mbele yetu kuna nini tutajua,” alisema.
“Hatuwezi kuweka nguvu yetu nje ya timu, walimu na wachezaji tunajua kazi yetu ni ipi, hivyo tunachopambana kwa sasa ni kushinda mechi mbili zilizobaki,” alisema.
Simba iko katika nafasi ya pili ya Ligi kuu Bara ikiwa na pointi 62 sawa na vinara wa ligi hiyo Yanga ambao ndiyo mabingwa watetezi.
Yanga wana wastani mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa au GD na wana mchezo mmoja zaidi ya Simba ambao unaonekana kubaki kuwa silaha kuu kwao,
0 COMMENTS:
Post a Comment