May 11, 2017Wakati bado ulimwengu wa michezo ukijadiliana namna Singida United Fc ilivyowanasa wazimbabwe Muroiwa na Kutinyu walioongoza kikosi cha timu yao ya Taifa pale Gabon kwenye michuano ya  AFCON 2017.

Hii leo kupitia chanzo chetu cha uhakika mjini NAIROBI kenya zinasema, Singida United Fc jana usiku walifanikiwa kuinasa saini ya beki kisiki wa timu ya Taifa ya UGANDA ambaye aliongoza safu ya ulinzi ya timu ya Taifa ya Uganda kwenye michuano ya AFCON 2017 pale Gabon.

 Mmoja ya wajumbe wa kamati ya usajili ya Singida United Fc ndg. Festo Sanga ametua jana Nairobi kumalizana na mchezaji huyo SHAFIK BATAMBUZE (23) anayekipiga TUSKER FC ya Kenya.

Shafik msimu uliopita alikuwa ni mchezaji bora wa ligi ya kenya kwa kuipatia ubingwa Tusker wa FA CUP na Premier League.

Kwa usajili huu, Singida United wameshafisha wachezaji wakimataifa 4 ambao wote wapo kwenye timu zao za Taifa,watatu ni kutoka zimbabwe(Elisha Muroiwa, Wisdom Mtasa na Twafaza Kutinyu) na sasa Mganda Shafik Batambuze.


Picha ni Shafik Batambuze alikubali kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Singida United Fc, hapa akiitumikia timu yake ya Tasker Fc .

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV