May 20, 2017


MPIRA UMEKWISHAAAA
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
DK 89 Ndemla anapiga kichwa safi kabisa lakini Kado anaokoa vizuri na mwisho inakuwa kona isiyo na manufaa
DK 85, shambulizi kali la Mwadui lakini mwamuzi anasema walikuwa wameishaotea
Dk 80 sasa, Simba wametawala zaidi katikati na Mwadui FC wamerudi nyuma kabisa wakionekana kufanya mashambulizi ya kushitukiza huku Simba wakiwa wameshindwa kuipenya ngome ya MWadui
Dk 75, Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini anapiga juuuuu
Dk 70, nafasi nzuri kwa Simba, lakini Athanas anang'ang'ania mpira bila sababu, Cholo anaokoa vizuri kabisa 
SUB 67, Pastory Athanas anaingia upande wa Simba kuchukua nafasi ya Ajibu
Dk 66, Muzamiru anaachia mkwaju mkali lakini Kado anafanya kazi ya ziada, anaokoa inakuwa kona. Yuko chini anatibiwa
DK 65 Simba wanapata kona ya sita, Kichuya anapiga kona fupi kwa Bukungu , Juuko anaachia mkwaju mkali lakini, kipa Shabani Kado yuko makini
SUB  DK 61 Salim Kabunda anaingia kuchukua nafasi ya Hassan Kabunda upande wa Mwadui FC
Dk 56, Simba wametawala zaidi katikati ya uwanja lakini hakuna mashambulizi makali


SUB Dk 53, anaingia Mwinyi Kazimoto na kuchukua nafasi ya Laudit Mavugo
Dk 48, Miraji anaachia mkwaju lakini Agyei anaonekana yuko makini
Dk 47, Simba inafanya kona ya kwanza kipindi cha pili, inachongwa lakini haina madhara
Dk 46 Mwadui FC wanaonekana kujibu mashambulizi lakini bado hakuna utulivu
Dk 45, Simba wanaonekana kuanza kwa kasi zaidi, hii inaonekana wanataka mabao ya haraka
SUB Dk 45 Ndemla ndani ya nyumba, anachukua nafasi ya Liuzio

MAPUMZIKO
-Chollo anaachia mkwaju mkali hapa lakini Agyei anadaka vizuri kabisa
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Mwadui wanaonekana kucharuka zaidi na kugongeana vizri katikati ya uwanja
GOOOOOOOOO Dk 44, anaachia mkwaju mkali baada ya kupokea pasi nzuri ya Kabunda na kuandika bao safi
Dk 42 Nonga anajaribu shuti kali kabisa lakini Agyei anadaka vizuri kabisa
Dk 39, Shuti la Mavugo linamgonga Mngeveke na kuwa kona, inachongwa hapa na kuondoshwa na Awadhi Juma
Dk 38 mpira unaendelea tena na Simba wanaonekana kuzidi kutawala


Dk 37, mpira umesimama, waamuzi wanajadili jambo hapa
Dk 32, nafasi nyingine nzuri kwa Simba lakini Kichuya anashindwa kuwa makini anashindwa kufunga
Dk 31 sasa, Simba wanaonekana kuutawala mpira kwa sasa hasa katika eneo la katikati ya uwanja
Dk 28, Kabunda anazunguka vizuri na kuachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango
GOOOOOOOOOOO Dk 25, Ajibu anaiandikia Simba bao la pili baada kugongeana vizuri na Liuzio anampa pasi nzuri kabisa
Dk 23 Awadhi Juma anaachia mkwaju mkali kabisa lakini goal kick


Dk 21, Mavugo anaachia mkwaju mkali, kipa wa Mwadui anapangua na kuwa kona. Inachongwa hapa haina manufaa
GOOOOOOOOOOOO Dk 18 Kichuya anafunga mkwaju wa penalti na kuiandikia Simba bao la kwanza 
PENAAAAAAAAAAT....Dk 16 Simba wanapata penalti baada ya kipa Shabani kumgonga Kichuya, wachezaji Mwadui wanamzonga mwamuzi
Dk 14, Mavugo anatoa pasi safi kwa Kichuya akiwa katika nafasi nzuri anajaribu kufunga, unaokolewa na kuwa kona. Inachongwa hapa lakini haina madhara
Dk 13, Mwadui wanajichanganya na Mavugo anajaribu lakini kipa anaokoa

Dk 12 sasa, Mwadui FC ndiyo wanaoonekana kuutawala zaidi mpira hasa katika eneo la katikati na Simba wako nyuma wakifanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 8 Ajibu anatoa pasi safi kabisa kwa Mavugo lakini Mavugo yeye na kipa, anachelewa
Dk 8, Mwadui wanafanya shambulizi kali kupitia awadhi Juma na kupata kona, inachongwa lakini wanaokoa
Dk 2, Simba wanajibu mashambulizi lakini krosi nzuri ya Ajibu haina mwenyewe, goal kick

Dk 1, Mwadui ndiyo wanaonekana kuanza kwa kasi kama wamepania kupata bao la mapema

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic