May 13, 2017





MPIRA UMEKWISHA 
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA 
Dk 89, Yondani anaonekana ameumia pale lakini anaamka Dk 87 sasa, inaonekana City wamepoteza mwelekeo, kwa kuwa hawana mipango ya uhakika na Yanga wanaonekana kuwadhibiti vizuri
Dk 84, Bossou analazimika kutoa mpira na kuwa kona, inachongwa lakini haina faida kwa City
Dk 79 Kakolanya anafanya kazi ya ziada akiwa Kenny, anapangua mpira vizuri kabisa
DK 77, City wanapata kona baada ya Ngassa kuwachambua mabeki wa Yanga
Dk 73, mpira wa adhabu wa Shamte unaunganishwa vizuri na Nchimbi, goal kick
SUB Dk 68, Cannavaro anakwenda benchi, nafasi yake inachukuliwa na Kelvin Yondani, kitambaa cha unahodha anamkabidhi Niyonzima


Dk 65 GOOOOOOOOOO mpira wa adhabu wa Juma Abdul, Chirwa akiwa ameachwa na mabeki wa Mbeya City, anaruka na kuupachika wavuni, Yanga mbili
Dk 64, mabeki wa Mbeya City wanalazimika kumfanyia madhambi Chirwa aliyekuwa amewatoka, faulo inapigwa na Juma Abdul
Dk 63, Nchimbi tena anamtoka Bossou lakini Kakolanya anakuwa makini
DK 62, nafasi nyingine nzuri kwa City lakini Yanga wanaonekana wako makini
SUB Dk 59, City wameamua kuongeza nguvu kwa kumuingiza Mrisho Ngassa na kumtoa Rajab Isihaka
GOOOOOOOOOO Dk 57 Shamte anaifungia City bao la kusawazisha, ni baada ya Nchimbi kumchambua Bossou aliyeanguka na kufunga bao la pili
Dk 56 sasa, Yanga wanaonekana kuupoza mchezo taratibu sana


SUB Dk 53, Kessy anakwenda benchi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin
Dk 52 krosi safi ya Juma Abdul lakini kipa Owen anadaka kwa ustadi mkubwa
Dk 51 nafasi nzuri kabisa kwa Kessy, lakini shuti lake linakuwa nyanya kwa Owen
Dk 48, krosi safi ya Juma Abdul, Tambwe anajitwisha hapa lakini unapita juuu
SUB Dk 46 Bryson Raphael anaingia kuchukua nafasi ya Zahoro Pazi upande wa City
Dk 45 Mpira umeanza, City wanaonekana kuwa na kasi wakitaka kusawazisha

MAPUMZIKO
-Krosi nzuri ya Juma Abdul, inaokolewa na kuwa kona, inachongwa na Mwashiuya, kona tena, kipa Owen anadaka kwa uzuri kabisa

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45 sasa, mpira unachezwa katikati ya uwanja zaidi
Dk 43, mpira wa adhabu, MWashiuya anaachiwa mkwaju hapa lakini inakuwa nyanya kwa kipa Owen Chaima
Dk 41, Kenny Ali, akiwa katika nafasi nzuri, peke yake, anapiga shuti kuuubwaaa
Dk 39, Kessy anachambua hapa, MWasapili anatoa na kuwa kona. Inachongwa vizuri lakini City wanaokoa vizuri kabisa


Dk 36, krosi safi ya Kessy, Tumba anaruka na kupiga kichwa mbali kabisa
Dk 33, Majaliwa analala kuokoa mpira wa Kessy na kuwa kona lakini haina manufaa kwa Yanga
Dk 33, Kessy analazimika kutoa mpira nje na kuwa kona. Nchimbi alikuwa anakwenda kwa kasi kumuona Kakolanya
Dk 29, Kona nyingine ya Isihaka Yanga wanaokoa na kuwa kona tena, inachongwa kona nyingine, Kakolanya anaokoa maridadi kabisa
Dk 28 krosi ya Majaliwa inaokolewa na kuwa kona, inachongwa na Rajab Isihaka na Kakolanya anafanya kazi nzuri kabisa hapa
Dk 25 sasa, City wanaonekana kuutawala mchezo, lakini kwa pasi nyingi katikati ya uwanja, hakuna mashambulizi makali


Dk 22, nafasi nyingine kwa Mbeya City lakini Alpha anaachia shuti kuuubwaaa
Dk 20 Nchimbi yeye na kipa wa Yanga lakini anapiga shuti mtoto kabisa hapa
Dk 17 Alpha anaachia mkwaju mkali hapa, lakini halikulenga lango
Dk 16 kona nyingine, inachongwa tena lakini City wanaokoa tena, Mwasipili anaosha hapa
Dk 14, Yanga wanapata kona, inachongwa vizuri na MWashiuya lakini City wako makini
Dk 13 Kenny Ali anaaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini Kakolanya anadaka vizuri kabisa
SUB Dk 12 Juma Abdul anaingia kuchukua nafasi ya MSuva ambaye ameshindwa kuendelea


Dk 10 Msuva anatolewa nje baada ya kutibiwa na jobo la madaktari
Dk 9, Msuva bado anatibiwa hapa baada ya kuumia. 
Anatibiwa kwa muda kidogo
GOOOOOOOOOO Dk 7, Msuva anaiandikia Yanga bao la kwanza kwa kufunga bao safi kabisa 
Dk 6, Ditram Nchimbi anashindwa kutulia, lakini inaonekana bado Mbeya City hawajaamka
Dk 3, mpira mzuri wa Bossou unamfikia Niyonzoma lakini hakuwa makini

Dk 1, mechi imeenza kwa kasi sana na Yanga wanaonekana wamepania kushinda

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic