May 13, 2017Kelvin Sabato amefunga bao pekee ambalo limeipa ushindi muhimu Majimaji ya Songea ambayo imeshinda 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.Mechi hiyo imepigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na ulikuwa mkali na wa kuvutia licha ya JKT kuwa tayari wameishateremka daraja.

Matokeo hayo yanaifanya kupata ahueni baada ya kufikisha pointi 32 na kujiondoa kwenye lile janga la kushuka daraja.

Hata hivyo, bado hawajawa na uhakika hadi watakaposhinda mechi ijayo ambayo itakuwa ni ya mwisho wao.

MATOKEO MENGINE
Prisons 2-1 Ndanda
Mtibwa 4-2 Mwadui

JKT 0-1 Majimaji
Kagera 2-1 Mbao FC

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV