May 6, 2017Nyota wa zamani wa Yanga, Edibily Lunyamila anaamini iwapo kiungo wa pembeni wa timu hiyo atapewa nafasi ya kutosha atafanya maajabu.

Lunyamila amesema Emmanuel Martin ni moja ya wachezaji wazuri ambao wanapaswa kupewa muda wa kucheza zaidi.

“Sitaki kuingilia uamuzi wa kocha lakini namuona Martin ana vitu fulani hivi. Anaweza kuongeza kujiamini kutokana na kuendelea kucheza.

“Kama atacheza kwa muda wa kutosha maana yake ataongeza kujiamini na kiwango chake kitapaa, kocha ampe nafasi zaidi,” alisema.

LUNYAMILA

Mara nyingi kocha wa Yanga, George Lwandamina amekuwa akimtumia Martin kama mchezaji wa akiba na amekuwa akimuingiza dakika chache za mwisho.


Martin ambaye amejiunga na Yanga akitokea JKU ya Zanzibar, amekuwa akionyesha uwezo mkubwa kila anapopata nafasi.

Yanga inashuka dimbani leo kwa ajili ya kuivaa Prisons katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV