May 5, 2017


Mbao FC ina uhakika wa kufanya vizuri na kubaki Ligi Kuu Bara na kazi hiyo inaanza kesho Jumamosi.

Mbao ina imani mechi yao dhidi ya Azam FC ugenini, tena usiku itakuwa ngumu lakini watafanfa vema.
“Itakuwa mechi ngumu lakini sisi tunataka kushinda na tumejiandaa kufanya vizuri.
“Tunajua Azam FC sasa wanataka heshima na watacheza kwa juhudi lakini watu waje waone naamini itakuwa mechi nzuri,” alisema Meneja wa Mbao FC, Joseph Constantine.
Mbao FC ina pointi 30 zinazoifanya ishikilie nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ambayo bado si nafasi salama.

Kama itashinda leo, basi itakuwa imejiweka katika nafasi nzuri kujikwamua kutoka katika eneo hilo na inaweza kupaa hadi katika nafasi ya 9 au 8.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV