May 6, 2017


Mshambuliaji nyota wa Yanga, Simon Msuva wa Yanga ana mabao 12 katika Ligi Kuu Bara sawa na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting, winga huyo huyo amepiga mkwara akisema hatishwi na kasi ya wafungaji wenzake katika ligi hiyo.

Ukiachana na Abdulrahman, Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar na Shiza Kichuya wa Simba, nao wana mabao 11, yaani moja pungufu ya yale yaliyofungwa na Msuva.

Amesema hatishwi na kasi ya ufungaji ya wapinzani wake hao isipokuwa yeye anapambana kuhakikisha anafunga zaidi ili kuongeza mabao yake.

“Kufunga ni kazi yao, hakuna haja ya kuwaogopa kwani na mimi nitapambana kuhakikisha nafunga kila ninapopata nafasi na si zaidi ya hapo, sina hofu wala hao wafungaji wengine hawanitishi.

“Mchezaji unatakiwa ujiamini kwa kile unachokifanya pia kumuomba Mungu kwa kila hatua mahali popote pale, sasa naamini nitafunga mabao mengi na kuwa mfungaji bora.


“Katika maisha huwezi kupata kitu kirahisi pasipo kupambana kwa uwezo wote, naamini kila kitu kinawezekana hivyo nitamuomba Mungu anijaalie ili maumivu yanipitie mbali tu,” alisema Msuva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV