Bradley Lowery ni kijana shabiki wa Sunderland ambaye amekuwa akipambana na ugonjwa wa kansa.
Desemba mwaka jana wazazi wake walielezwa wazi kwamba matibabu watakayofanya nchini Marekani yatasaidia tu kupeleka mbele maisha ya kijana huyo lakini hatapona.
Bradley amekuwa karibu na mshambuliaji nyota wa Sunderland, Jermaine Defoe.
Mara zote kijana huyo na familia yake ya Lowery hawajachoka kuwashukuru mashabiki, uongozi na wadhamini wa Sunderland kwa upendo ambao wamekuwa wakimuonyesha.
0 COMMENTS:
Post a Comment