Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makala ameipongeza Kampuni ya Coca Cola kwa kudhamini michezo kwa muda mrefu na kusaidia kuibua vipaji vingi ikiwemo vijana wanaocheza timu ya taifa chini ya miaka 17, Serengeti Boys.
Vifaa vilivyotolewa ni kwa ajili ya sekondari zote mashindano ya Umiseta mpira wa miguu na kikapu.
Makala ambaye ni mpenda michezo amewataka Eaofisa Elimu na walimu wa michezo kuendeleza michezo mashuleni.
Aidha, amewaagiza mabaraza ya madiwani kulinda viwanja vya shule visivamiwe na shule zisizo na viwanja halmashauri zitenge maeneo ya michezo kwa shule zisizo na viwanja.
Wakati akiwa bungeni, makala alikuwa nahodha wa timu ya wabunge na akiwa kiungo mkabaji au mkataba umeme tegemeo kabisa.
0 COMMENTS:
Post a Comment