May 24, 2017



Kikosi cha Simba, kimeamua kujificha mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wao wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC, unaotarajiwa kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Simba ambao wapo Morogoro, wameamua kuweka kambi maeneo ya Nane Nane ambapo awali walikuwa hapo walipokuwa wakijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1. 

Mchezo huo ulipigwa Februari 25, mwaka huu.

Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja raia wa Uganda, amesema kitu kinachompa matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo wao huo ni kutokana na hali za wachezaji wake kuwa nzuri.

“Bado tupo Morogoro tukiendelea na maandalizi yetu ya mchezo wa fainali dhidi ya Mbao, mchezo huo hatuuchukulii rahisi kwa sababu kama ujuavyo fainali ni fainali, lolote linaweza kutokea.

“Leo (jana) asubuhi tumefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Jamhuri, vijana wangu wapo safi hakuna hata mmoja mwenye majeraha na tunatarajia kwenda Dodoma Alhamisi (kesho) au Ijumaa.


“Tutaenda kupambana na Mbao tukifahamu kwamba wameweza kuifunga Yanga mara mbili, hivyo ni lazima na sisi tujipange kisawasawa kuhakikisha hatupati aibu kama iliyowapata wapinzani wetu,” alisema Mayanja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic