May 11, 2017Uongozi wa klabu ya Yanga umewaambia wachezaji wake wanaotaka kuondoka katika kikosi chake, “Wanaweza kwenda”.

Imethibitika zaidi ya wachezaji watano wa Yanga, mikataba yao inaisha mwishoni mwa msimu na Yanga imesema kama kuna anayetaka kuondoka hata kama ni kujiunga na Simba, “ruksa”.

Mmoja wa wachezaji waliokuwa wakihusishwa na kujiunga na Simba ni Donald Ngoma ambaye ni mshambulizi kutoka nchini Zimbabwe.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema wamezungumza na wachezaji na kuwaeleza.

“Sikia, tumezungumza na wachezaji na kuwaeleza. Sisi kwa sasa tutabaki na mtu ambaye anataka kubaki Yanga.

“Kama kuna mchezaji anataka kuondoka, sawa, ruksa. Lakini kama anataka kubaki tutakaa na kujadili tujue tufanye nini kuongeza mkataba,” alisema Mkemi akizungumza katika kipindi cha SPOTI HAUSI kinachorushwa na runinga ya mtandaoni ya Globaltvonline.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV