May 28, 2017





Shabiki mmoja amefariki dunia katika ajali ya gari katika eneo la Dumila mkoani Morogoro, ndani ya gari hilo alikuwamo nahodha wa Simba, Jonas Mkude.

Mkude ni kati ya majeruhi na wengine watatu pia wameumia na tayari wako njiani wakitoka Dumila kupelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro.


Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Muslah Al Rawah amethibitishwa kwa majeruhi hao kupelekwa Morogoro.

 Mkude alikuwa njiani kutoka Dodoma kurejea Dar es Salaam baada ya jana Simba kuitwanga Mbao FC kwa mabao 2-1 na kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho.


Mkude alikuwa katika gari na baadhi ya mashabiki wa Simba na gari lilipasuka tairi na kuanguka. Mtu mmoja amefariki dunia.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic