May 10, 2017Klabu ya soka ya Yanga inapenda kuwatangazia wanachama, wapenzi, mashabiki na wadau wa soka jijini Dar es salaam sanjari na mikoa ya karibu kwamba; mchezo wa Jumamosi kati ya Yanga SC  na Mbeya City utachezwa uwanja mkuu wa taifa  usiku badala ya kuanza saa 10:00 kama ilivyo ada. 


Mchezo huo utaanza majira ya saa 12:00 jioni na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kongwe kabisa nchini kucheza mchezo wake wa ligi kuu usiku katika miaka ya hivi karibuni. 

Maamuzi haya yamezingatia matakwa na masilahi ya wadau wa soka nchini ambao wana kiu na hamu ya kuutazama mchezo huo lakini pia wakiwa ni sehemu ya wadau wa mchezo wa riadha itakayofanyika uwanja wa taifa jumamosi hiyo hiyo. 

Tunawaomba wanachama na mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti vijana wao kwani ulinzi utakuwa imara na thabiti.

Nyote mnakaribishwa

Imotolewa na Idara ya habari na mawasiliano
Young aAfricans Sports Club

10.05.2017

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV