June 13, 2017


Mshambuliaji mpya wa Simba, John Raphael Bocco, yuko tayari kuanza kazi yake na kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.

Bocco amejiunga na Simba akitokea Azam FC ambayo imeamua kubana matumizi.

Straika huyo mkongwe amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba ina nafasi ya kuutumia uzoefu wa Bocco wa zaidi ya misimu saba kwenye Ligi Kuu Bara.


Naye anaonekana yuko tayari na kazi baada ya kukabidhiwa jezi yake rasmi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV