June 12, 2017



Uongozi wa Singida United umemuandalia mkataba kiungo mshambuliaji wa Yanga, Deus Kaseke kwa ajili ya kuusaini huku wakimwambia apumzike kwanza kabla ya kuusaini.

Kaseke ni kati ya wachezaji 13 waliopo kwenye orodha ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika mwishoni mwa msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara.

Wachezaji wengine baadhi ambao mikataba yao imemalizika ni Haruna Niyonzima, Vincent Bossou, Deogratius Munishi 'Dida', Thabani Kamusoko, Anthony Matheo na Malimi Busungu.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya uongozi wa Singida, kiungo huyo amepewa muda wa mapumziko baada ya kumaliza ligi kuu na kuahidiwa kupewa mkataba wa kuichezea timu hiyo.
Chanzo hicho kilisema, kiungo huyo tayari amewatajia dau la shilingi milioni 40.
"Kaseke tupo kwenye mazungumzo naye ya mwisho kwa ajili ya kusaini mkataba wa miaka miwili na alitakiwa asaini tangu mwezi uliopita na kikubwa tulitaka kumpa muda wa mapumziko kwa ajili ya kutuliza akili yake kabla ya kusaini.

"Tunamsajili Kaseke baada ya kupewa mapendekezo na kocha wetu Pluijm (Hans) aliyokabidhi hivi karibuni," kilisema chanzo hicho.

Alipotafutwa Kaseke kuzungumzia hilo, alisema: "Ni kweli Singida walinifuata kwa ajili ya mazungumzo ambayo bado hatujafikia muafaka kwa maana ya kusajili, lakini kila kitu kingine kinaenda vizuri.”

Kwa upande wa Pluijm alipotafutwa kuzungumzia usajili wa Kaseke alisema: "Nimepanga kuongeza wachezaji sita pekee kati ya hawa nilionao, tayari nimekabidhi mapendekezo yangu kwa uongozi na muda ukifikia nitakutajia majina ya wachezaji hao, kama unavyojua ukimtangaza mchezaji hivi sasa kabla ya kumalizana naye klabu hizi kubwa nazo zitamtaka.” 

Katika kikosi cha Singida, Kaseke atapata nafasi ya kufundishwa tena na Pluijm ambaye alikuwa kocha wake Yanga.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic