June 13, 2017

PIUS BUSWITA AKIMILIKI MPIRA MBELE YA IBRAHIM AJIBU WA SIMBA

Wakati kumekuwa na taarifa kwamba Pius Buswitaameishasaini Yanga, sasa ni uhakika kiungo huyo wa Mbao FC, amejiunga na mabingwa wa Kombe la Shirikisho, Simba.

Simba imefanikiwa kumsainisha Buswite kimyakimya na kuwapiga bao Yanga na Azam FC walioonekana kumhitaji. Kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka miwili.

Mchana wa leo kumekuwa na taarifa Buswita amejiunga na Yanga lakini taarifa zimeeleza, Yanga walimpa kishika uchumba tu, wakati Simba ndiyo waliofanikiwa kumsainisha.
“Kweli Buswita amesaini Simba na sisi tunajua, tayari ameaga na kila kitu kimekwenda vizuri,” alisema mmoja wa viongozi wa Mbao FC.
Kiungo huyo alionyesha uwezo mkubwa wakati wa michuano ya Kombe la Shirikisho, ikiwemo mechi ya fainali dhidi ya Simba.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV