June 22, 2017Sasa ni uhakika kwamba Emmanuel Okwi anakuja nchini kumalizana na Simba kwa ajili ya kuanza kuichezea msimu ujao.

Okwi anatarajia kutua nchini Jumamosi na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe maarufu kama ZHP amethibitisha.

Hans Poppe amewaambia waandishi wa habari leo kwamba Okwi anakuja kumalizana na Simba na kazi itakuwa ni kusaini.


“Anakuja Jumamosi, hapa ni suala la kusaini kwa kuwa suala la mazungumzo tulimaliza Kampala,” alisema Hans Poppe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV