June 23, 2017Baada ya shabiki mmoja wa Yanga kuonekana akiichoma moto jezi ya kiungo Haruna Niyonzima.

Niyonzima raia wa Rwanda, ameamua kuondoka Yanga baada ya mkataba wake kwisha na klabu ya Yanga ikawa haina fedha ya kumsajili tena kutokana na dau lake aliloweka mezani.

Mjadala mkubwa mitandaoni ni namna ambavyo shabiki huyo amechoma jezi hiyo akionyesha hasira kwa kuwa Niyonzima ameamua kuondoka na kuna taarifa kwamba anakwenda Simba.

Mashabiki kadhaa wamekuwa wakimuunga mkono aliyefanya hivyo. Lakini wako wengi ambao wamekuwa wakimpiga, wakiamini si jambo sahihi.

Mjadala huo unaonekana kuwa mkali na kuna sehemu watu wanashindwa kuthibiti jazba zao kwa kuanza kutoa maneno makali.

Mjadala huo ulianza jana jioni mara tu baada ya picha mnato na zile za videoza shabiki akichoma jezi, zilipoanza “kutambaa” mitandaoni.


1 COMMENTS:

  1. Mimi ni shabiki wa Yanga,ika siungi mkono uchomaji wa jezi ya Haruna.Ikumbukwe mpira ni kazi yake,na anachoangalia ni masilahi ya maisha yake.Aachwe aende kama kweli club imeshindwa kutimizamatakwa yake

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV