June 22, 2017




Kozi ya waamuzi wa mpira wa miguu, iliyolenga kuwainua  madaraja kutoka madaraja waliyonayo sasa hadi ngazi moja juu, imesogezwa mbele kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Salum Chama.

Chama amesema kwamba kozi hiyo iliyopangwa kufanyika kuanzia Juni 29, mwaka huu itafanyika hapo baadaye katika tarehe itakayopangwa, lakini itakuwa ni kabla ya  Uchaguzi Mkuu wa TFF.


“Watu wasiende kuripoti hiyo Juni 29, mwaka huu kama tulivyotangaza. Tumesogeza mbele kidogo kozi hii. Tarehe mpya itatangazwa hapo baadaye,” amesema Chama ambaye alitaja vituo vilivyopangwa kuwa ni Mwanza, Ruvuma na Dodoma.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic