Mshambuliaji nyota wa Barcelona, Lionel Messi amekanusha na kukataa katakata kwamba alitumia pauni 35,000 (Sh milioni 98), kwa ajili ya vinywaji na chakula.
Taarifa zilizosambaa mitandaoni, zimeeleza Messi ametumia fedha hizo kwa ajili ya vinywaji na chakula akiwa na marafiki zake, Cesc Fabregas na Luis Suarez wakiwa na wake zao.
Watu sita hao, wake katika mapumziko huko Ibiza nchini Hispania na taarifa matumizi hayo zilisambaa mitandaoni.
Messi ametupia maneno mtandaoni akionyesha kushangazwa na taarifa hizo huku akisistiza ni uzushi lakini ameshangazwa na watu uamini.
Usiku huo Messi anaonekana akiwa na mpenzi wake wa siku nyingin, Antonella Roccuzzo wakati Fabregas alikuwa na Daniella Semaan na Suarez kama kawaida na Sofia Balbi.
Kuna taarifa kwamba lisiti hiyo ya TRA ya Hispania ilichezewa kabla ya kuonyesha kuwa Messi alifanya matumizi hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment