June 11, 2017


Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire haishi vituko. 

Leo amekuwa kivutio wakati wa fainali ya SportPesa Super Cup ambayo imewakutanisha watani wa Kenya, AFC Leopards dhidi ya Gor Mahia ambao wameshinda kwa mabao 3-0 na kuwa mabingwa.

Masau aliibuka uwanjani hapo akiwa na simu zake tano mkononi.

Hali hiyo ilionyesha kuwashangaza wengi na hasa mashabiki kutoka Kenya ambao hawajamzoea.

Kama haitoshi, Masau alikuwa akionyesha umahiri wa kupokea moja baada ya nyingi kila zilipoita na kufanya gumzo huku watu wengine wakicheka.


Masau anamiliki simu tano kwa wakati mmoja na kila moja inatumika na amewahi kusema angependa ziwe zaidi ya hizo

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV