June 25, 2017


Unaweza usiamini, jana tu ilitolewa zawadi ya mtaa, asubuhi ya leo tayari bango la Mtaa wa Victorr Wanyama limeng’olewa.

Taarifa zinaeleza wako ambao walitakiwa kuba bango hilo kwa ajili ya vyuma chakavu lakini wengine wanaeleza, wako waliochukizwa Wanyama kupewa jina la mtaa Tanzania.

Jana, Meya wa Manispaa ya Ubongo Boniface Jacob, alimtunuku mtaa, Kiungo wa Tottenham ya England Victor Wanyama raia wa Kenya.

Jacob ambaye ni Meya akitokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alimkabidhi Wanyama mtaa ambao awali ulikuwa unajulikana kama Viwandani na sasa utajulikana kama Victor Wanyama.


Mtaa huo uko Ubungo katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.1 COMMENTS:

  1. Sasa mtaa mwingine mwambie I huyo meya mshamba amle mahmadou shako maana ameenda kutazama mechi ya kumuaga ninja kwenda tanga

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV