Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani amejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania
urais wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
Nyamlani aliwasilisha barua TFF leo Jumapili Juni 25, mwaka
huu ikiwa ni siku moja tu tangu Kamati ya Uchaguzi ipitishe jina lake kuwa
miongoni mwa wagombea 10 wanaowania nafasi hiyo ya urais. Sababu aliyoeleza ni
masuala binafsi.
Kwa msingi huo, wagombea wanaobaki kwenye kinyang’anyiro na
kuhitajika kufika kwenye usaili kuanzia Juni 29, mwaka huu ni tisa wakiongozwa
na Rais wa sasa, Jamal Malinzi anayetetea nafasi.
Mbali ya Malinzi wengine wanaowania nafasi hiyo ni Imani
Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe,
Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.
Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako
Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert
Selasela na Stephen Mwakibolwa.
Mbali ya nafasi za urais na makamu rais, Abdallah Mussa -
aliyekuwa akiwania nafasi ya kugombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji TFF kutoka
Kanda Na. 1 (Mikoa ya Kagera na Geita) aliondolewa kwa sababu ya
kutoambatanisha kivuli cha cheti ya elimu ya sekondari.
Hivyo wagombea wa nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji
kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:
Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;
Soloum Chama
Kaliro Samson
Leopold Mukebezi
Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;
Vedastus Lufano
Ephraim Majinge
Samwel Daniel
Aaron Nyanda
Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;
Benista Rugora
Mbasha Matutu
Stanslaus Nyongo
Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;
Omari Walii
Sarah Chao
Peter Temu
Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;
John Kadutu
Issa Bukuku
Abubakar Zebo
Francis Michael
Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;
Kenneth Pesambili
Baraka Mazengo
Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;
Elias Mwanjala
Cyprian Kuyava
Erick Ambakisye
Abousuphyan
Silliah
Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;
James Mhagama
Golden Sanga
Vicent Majili
Yono Kevela
Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;
Athuman Kambi
Dunstan Mkundi
Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;
Hussein Mwamba
Mohamed Aden
Musa Sima
Stewart Masima
Ally Suru
George Benedict
Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;
Charles Mwakambaya
Gabriel Makwawe
Francis Ndulane
Hassan Othman
‘Hassanol’
Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga
Khalid Mohamed
Goodluck Moshi
Thabit Kandoro
Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam
Emmanuel Ashery
Ayoub Nyenzi
Saleh Alawi
Shaffih Dauda
Abdul Sauko
Peter Mhinzi
Ally Kamtande
Said Tully
Mussa Kisoky
Lameck Nyambaya
Ramadhani Nassib
Aziz Khalfan
Jamhuri Kihwelo
Saad Kawemba
Bakari Malima
0 COMMENTS:
Post a Comment