July 10, 2017


Kiungo kinda wa zamani wa Simba, Haji Ugando ameanza majaribio nchini Serbia.

Meneja wa wake, Jamal Kisongo amesema kwa kushirikiana na wakala maarufu barani Ulaya, amewasaidia kupata nafasi hiyo ya majaribio.

“Ameanza majaribio na ninaamini atafanya vizuri. Kama mambo yatakwenda vizuri basi watapata timu.

“Kikubwa tuvute subira na kujua mambo yameendaje na hapo nitakuwa la kusema,” alisema.

Kisongo ambaye ni meneja wa Mbwana Samatta amesema mchezaji mwingine ambaye alikuwa na nafasi hiyo ya majaribio ni Salim Mbonde.


“Mbonde ameamua kusajili Simba, lakini kabla alikuwa amepata nafasi na tumekubaliana,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV