July 2, 2017



Uamuzi wa wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutaka kuwakata wagombea kadhaa kama kulipa kisasi kukosekana kwa mgombea waliyemtaka ndiyo ilikuwa chanzo cha kuvurugika kwa mambo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli amesimamisha mchakato wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma.

Kuuli amesema alishindwa kuvumilia uonevu huku baadhi ya wajumbe wakitaka kukatwa kwa wagombea wengine bila ya sababu za msingi.

Taarifa nyingine zinaeleza, wajumbe walikuwa na wajumbe kadhaa waliotaka wakatwe.

“Inaonekana kulikuwa na maelekezo kwamba kuna wajumbe fulani lazima wasipite. Hivyo walitaka wakatwe lakini hakukuwa na vigezo vya kuwakata.

“Hivyo kukazuka mvutano, kumbuka jana kulikuwa na mvutano wa wajumbe kutaka Malinzi ambaye yuko mahabusu lazima afanye usaili. Hawakukubaliana na Malinzi kukosa usaili,” kilieleza chanzo.

Wakati Kuuli anaeleza uamuzi wake alisema: “Nimeona si sawa, nimeshindwa kuvumilia uonevu na wajumbe wanataka kuwakata wagombea bila ya sababu wala vigezo.
“Nimeona nina mamlaka ya kusimamisha mchakato wa uchaguzi na nimewasilisha TFF. Kama hii itaendelea sitakubali kuwa kwenye kamati ya namna hii,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic