July 2, 2017

SALIM "TRY AGAIN"


Salim Abdallah ambaye ni Mwenyekiti wa Friends of Simba, ndiye Kaimu Rais wa Simba.

Amechukua nafasi hiyo baada ya kuteuliwa na wajumbe wa kamati ya utendaji kukaimu kwa muda ingawa Kassim Dewji ndiye alikuwa ameteuliwa.

Salim maarufu kama Try Again anakaimu nafasi ya Evans Aveva ambaye yuko mahabusu akituhumiwa na kesi ya utakatishaji fedha.

Try Again ameikaimu nafasi hiyo baada ya Dewji aliyewahi kuwa katibu mwenezi na katibu mkuu Simba kukataa pale kikao cha kamati ya utendaji kilipokutana.

Dewji amekataa kwa kuwa ana majukumu mengi ya kifamilia lakini taarifa zinaeleza, hakutaka kuanzisha migogoro kwa kuwa kuna makundi yanampinga.


“Alijua kutaanza migogoro na yeye asingependa jambo hilo kufanyika kipindi hiki,” kilieleza chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV