July 11, 2017Everton FC ya England wamezitangaza rasmi jezi watakazozitumia watakapocheza kuivaa Gor Mahia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, keshokutwa.

Everton ambayo ilimaliza msimu uliopita wa Ligi Kuu England katika nafasi ya saba, itawavaa mabingwa wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia katika mechi inayosubiriwa kwa hamu kubwa.

Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu zaidi baada ya nahodha wa zamani wa Man United, Wayne Rooney kujiunga tena na Everton.

Lakini Gor Mahia inanolewa na kocha wa zamani wa Simba, Dylan Kerr ambaye tayari ameanza mazoezi na timu yake hiyo mpya.

Kerr raia wa England amejiunga na Gor Mahia wiki moja na nusu iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV