July 11, 2017


Kikosi cha Yanga, kimeanza mazoezi yake chini ya Kocha George Lwandamina kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Lwandamina raia wa Zambia ameanza kukinoa kikosi chake kipya kikiwa na wachezaji wapya kama Ibrahim Ajibu na Abdallah Haji Shaibu maarufu kama Ninja.


Mazoezi hayo yamefanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Yanga wakiwa wameanza safari ya msimu ujao wa 2017-18.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV