July 20, 2017



Tamasha la Majimaji Selebuka linalohusisha michezo mbalimbali linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumapili hii katika Viwanja vya Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.

Tamasha hilo litahusisha michezo ya riadha (kilomita 42, 21, 19, 5 na 2.5) Mbio za baiskeli, Ngoma za asili, Mbio za walemavu, Mdahalo kwa shule za sekondari utakaosimamiwa na Jata (Umoja wa Ushirikiano kati ya Japan na Tanzania), Utalii wa ndani pamoja na maonyesho ya bidhaa zinazopatikana mkoani Songea.


Mratibu wa Tamasha hilo la Majimaji Selebuka, Magoti Faustine amesema kuwa tamasha hilo litakuwa na sura mpya kwa mwaka huu ambao ni watatu tangu kuanzishwa kwake kutokana na kuwa na michezo mingi ambayo itatoa vipaji vya wanamichezo mbalimbali.

“Lengo kubwa la tamasha hili la Majimaji Selebuka ni kuvitoa vipaji vipya vya michezo mbalimbali, ambapo kuanzia Julai 23 (Jumapili hii) watu wataanza kuona wachezaji wapya wa michezo mingine tofauti na soka wakiibuliwa.

Majimaji Selebuka inafanyika kwa mara ya tatu mfululizo na limekuwa ni tamasha linalokua kwa haraka kwa upande wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Tamasha hilo hushirikisha michezo mbambali hasa baiskeli na kadhalika. Lakini kumekuwa na makongamano ya wanafunzi pia hutoa nafasi kwa wajasiliamali kuuza bidhaa zao mbalimbali huku ikikaribisha wadau kutoka nje ya Tanzania kushuhudia.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic