July 17, 2017

Kamati ya nidhamu ya TFF ambayo imeundwa hivi karibuni, huenda ikatoa msamaha kwa wale waliokuwa wamefungiwa.

Taarifa za ndani zinaeleza, Haji Manara na Dk Damas Ndumbaro ambao walifungiwa kwa figisu wanaweza kusamehewa.

“Kumekuwa na vikao kuangalia mambo yalivyokwenda na ilionekana kuwa Ndumbaro, Manara na hata Jerry Muro ambaye anamalizia adhabu yake walifungiwa kimakosa.

“Huenda wakaunguliwa, lakini ni suala la kusubiri tu,” kilieleza chanzo kutoka TFF.

Wote walifungiwa na utawala wa Malinzi ingawa walilalamika kwamba kufungiwa kwao ilikuwa ni suala la uonevu wa wazi.


Hata hivyo, uongozi wa Malinzi haukuonyesha kushitushwa na lawama zao pamoja na wadau mbalimbali kwamba walikuwa wakiwaonea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV