July 30, 2017Tecno Mobile ni mbia na timu ya mpira ya Manchester City Footbal Club kutokea nchini Uingereza,Tecno na Manchester City inasemekana wameamua katika kukuza uhusiano wao watoe simu maalumu inayooonesha lebo za simu hizi mbili. 

Ilitegemewa Tecno Kutumia uhusiano huu na klabu  hii maarufu katika biashara kwa kuleta bidhaa sokoni zilizo na uhusiano wa moja kwa moja na klabu hii ya mpira wa miguu kutokea nchini Uingereza ili kukuza soko lake, ndivyo  ilivyotokea kwani Tecno wameingia kazini na picha zinaaanza kujieleza. 

Uchaguzi wa  simu itakayotumika kwa ajili ya ushirikiano huu ni sahihi, kama ulikua haujui Tecno  Camon CX, ni mfululizo wa matoleo ya camon yanakuja na kamera kali Zaidi ikiwa ni ya tatu katika  matoleo yake.


KAMERA KALI:- Ina kamera yenye  16mp mbele , ikiwa na uwezo wa kupiga  picha katika mwanga mdogo lakin pia flashi mbili mbele zinazosaidia kupiga picha  za mbele nnzur maarufu kama selfie. 

kamera ya nyuma inapiga Picha kwa haraka Zaidi. 
Lakini pia mafaili yatakua salama kwasababu simu hii imewekewa usalama wa alama za vidole, lakini hii ya usalama wa vidole haiji kwaajili ya kazi moja tu ila pia itatumia kupigia picha kwa haraka Zaidi kwa spidi ya 0.1 sec. 


MWONEKANO WA KIBABE: if nothing else about this phone gets your attention, its hardware will. The TECNO Camon CX Limited edition is a smartphone fit for the top flight and a worthy bearer of “The Citizens” crest. 

Kama hakuna kilichokushtua kuhusu simu hii basi muonekano wake utakubeba moja kwa moja. Tecno Camon CX  toleo  maalumu la klabu ya Manchester  City ni simu ya kijanja  inayokupa nafasi ya kua daraja la juu. 

Mwonekano wa mwisho wa simu hii unaonesha ni kwa jinsi gani simu janja hii  inakuja n amuonekano wa kibabe lakini ukiwa umebeba 64GB za kuhifadhi vitu ndani ya simu bila kutumia memori kadi ya nje huku ikipewa RAM ya 4GB inayotoa nafasi y akutumia Zaidi ya aplikesheni 50 kwa wakati mmoja.
.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV