July 14, 2017
Mambo safi kwa Ramadhani Singano maarufu kama Messi kwa kuwa ameishamalizana na klabu ya Difaa Al Jadida.

Kati ya leo au kesho, Singano anatarajia kuondoka nchini kwenda Morocco kujiunga na klabu hiyo.

SALEHJEMBE ilikuwa ya kwanza kukueleza, Singano aligoma kusaini mkataba wa Azam FC.

SALEHJEMBE ikawa ya kwanza kukueleza Singano ameanza mazungumzo na klabu hiyo ya Morocco na sasa inakuwa ya kwanza kukueleza kwamba walishamalizana.


Msimu uliopita, Al Jajida ilishika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Morocco maarufu kama Botola nyuma ya mabingwa, Raja Casablanca. Maana yake itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV