July 20, 2017

USENGIMANA

Kikosi cha Singida United, kimeendelea na mazoezi yake ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara.

Singida United chini ya Kocha Hans van der Pluijm iko jijini Mwanza ambako imeweka kambi.

Timu hiyo ambayo ni pekee inayodhaminiwa na SportPesa kutoka nje ya Dar es Salaam, imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mmoja wa wachezaji ambaye amekuwa ni kivutio katika mazoezi hayo ni mshambuliaji nyota aliyetokea Polisi Rwanda, Danny Usengimana.

Usengimana amekuwa mfungaji wa Ligi Kuu Rwanda kwa misimu miwili mfululizo.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic