July 20, 2017


Yanga imemnasa kiungo kinda mwenye kasi aitwaye, Baruani Yahaya Akilimali na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

Taarifa zinaeleza, Yanga wamefanya umafia na kumtwaa Akilimali ambaye ni mdogo wake na Yahaya Akilimali aliyewahi kuwa nyota wa Simba.

Kiungo huyo alielelezwa kuwa anasoma Uganda, alikuwa ameanza mazoezi na Lipuli ya Iringa kwa lengo la kusajiliwa kwa ajili ya Ligi Kuu Bara.

Lakini Yanga baada ya kugundua mchezo na kuona uwezo wake mazoezini, mara moja walifanya haraka na kumsajili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic