July 9, 2017


Kikosi cha Taifa Stars kimewasili nchini na kupokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harisson Mwakyembe.

Dk Mwakyembe aliwapokea Stars ambao wamewasili leo saa 9:30 alfajiri wakitokea Afrika Kusini walipokwenda kushiriki michuano ya Cosafa.
Stars wamefanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuing’oa Lesotho kwa mikwaju ya penalti katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV