July 9, 2017

Pamoja na kuwa gumzo kuhusiana na uhamisho wake kwenda Manchester United, ’Romelu Lukaku atapandishwa kizimbani nchini Marekani.
Mshambulizi huyo wa Everton aria wa Ubelgiji atapamba kizimbani Oktoba 2, mwaka huu katakana na usumbufu uliosababishwa na kelele zilizotoka katika jumba alilokodi katika eneo la Beverly Hills.

Amekamatwa wikiendi iliyopita baada ya majirani kulalamika kutokana na kelele hizo.
Kwa mujibu wa Polisi wa Beverly Hills, Lukaku alionywa mara tano kabla ya polisi hao kumuweka chino ya ulinzi.
Kwa Marekani na nchi za Ulaya, majirani wanaweza kushitaki kama mwingine anawasumbua kwa kelele.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV