July 12, 2017


Wapenda soka Raia wa DR Congo wanaoshi nchini, leo walijitokeza kwa wingi kumpokea mshambulizi nyota wa Everton, Yannick Bolasie.

Wengi walijitokeza kumpokea wakati akitua pamoja na kikosi cha Everton ambacho kipo nchini.

Baada ya Everton kutua, Wacongo hao walijipanga nje ya uzio wakimsubiri Bolasie ambaye anakipiha katika timu yao ya taifa.

Mara baada ya Bolasie kutokea, walimshangilia kwa nguvu wakiimba jina lake. Naye akaonyesha ni mwenye furaha akawapokea kwa kuwapungia mkono hali iliyozidisha shangwe.

Everton kesho watakuwa Uwanjani kuwavaa mabingwa wa SportPesa Super Cup, Gor Mahia katika mechi inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV