July 10, 2017


Staa wa soka wa Everton, Wayne Rooney amesema kuwa anatarajiwa kusafiri na timu yake hiyo kuja Tanzania kucheza mechi dhidi ya Gor Mahia chini ya udhamini wa Kampuni ya SportPesa.

Everton itashuka Dar es Salaam kukipiga dhidi ya Wakenya hao katika kukamilisha michuano ya SportPesa Super Cup ambayo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar na kushirikisha timu kadhaa.

Baada ya nahodha huyo wa zamani wa Manchester United, kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake, amesema kuwa atakuwemo kwenye msafara huo chini ya Kocha Ronald Koeman.

 
 Akiwa Everton, Rooney, 31 atakutana na Morgan Schneiderlin pamoja na Michael Keane ambao alicheza nao pamoja Manchester United, wakati Phil Jagielka, Leighton Baines na Ross Barkley amekuwa akikutana nao kwenye majukumu ya timu ya taifa.

“Naisubiri kwa hamu, naamini itakuwa safari nzuri, tutapata nafasi ya kucheza na kujuana, ni jambo zuri unaposafiri na timu, kuwa hoteli moja, kuwa pamoja muda mwingi, hiyo itasaidia kujuana vizuri.

“Sijawahi kufika Tanzania kabla naamini nitafurahia safari yangu,” amesema Rooney.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV