July 5, 2017


Nahodha wa Manchester United amekubali kujiunga na klabu yake ya zamani ya Everton FC baada ya wakala wake kukamilisha mazungumzo na klabu hiyo iliyomkuza.

Everton FC itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa SportsPesa Super Cup Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Taarifa zimeeleza kuwa Rooney amejiondoa katika safari ya kwenda Marekani ambako Man United itafanya mazoezi kujiandaa na msimu mpya.


Chanzo kutoka Old Trafford kimeliambia Gazeti la The Sun la Uingereza kwamba usiku wa kuamkia jana, kila kitu kilikamilishwa kuhusiana na makubaliano.
Akiwa na Man United, Rooney ametupia mabao 253 kambani na alijiunga nayo kwa kitita cha pauni milioni 26.5 miaka 13 iliyopita akitokea makao makuu ya Everton, Goodison Park.


Kabla kulikuwa na taarifa kwamba Rooney angekwenda Marekani au China kubeba mamilioni ya fedha lakini suala la familia yake kuishi nchini humo linaonyesha kutomfurahisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV