August 13, 2017
Baada ya kupoteza mechi iliyopita ya kirafiki dhidi ya JKT Ruvu, Yanga imeamka na kuichapa 2-0 Mlandege FC ya Zanzibar.

Mechi hiyo iliyopigwa visiwani Zanzibar, Yanga walionekana kuwa na mabadiliko makubwa katika ushambulizi.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Ibrahim Ajibu akiwa amefungua akaunti ya mabao visiwani humo na Emmanuel Martin akatupia la pili.


Kama Yanga wangekuwa makini wangeweza kufunga mabao mengi zaidi lakini nafasi kadhaa za wazi, walizipoteza.

Yanga imetua Zanzibar, inakwenda Pemba kwa ajili ya kuweka kambi kujiandaa na Ligi Kuu Bara lakini yakiwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuivaa Simba katika mechi ya Ngao ya Jamii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV