Kiungo Papy Kabamba Tshishimbi
tayari yuko nchini na ameungana na wenzake visiwani Zanzibar kwa
ajili ya kambi.
Yanga imepita
Unguja ikiwa njiani kwenda Pemba ambako itaweka kambo yake kabla ya kuivaa Simba
wikiendi ijayo katika mechi ya Kombe la Shirikisho.
Siku chache
zilizopita, Yanga walitangaza kupoteza mawasiliano ya Tshishimbi raia wa DR
Congo aliyekuwa anakipiga Mbabane Swallows ya Swaziland.
Lakini baadaye,
taarifa zinaeleza walimpata na ametua nchini tayari kusaini mkataba na
kumalizana na Yanga.
Mmoja wa viongozi
wa Yanga amesema, Tshishimbi ataanza mazoezi mjini Pemba na mara ya kwanza
ataonekana katika mechi dhidi ya Simba kuwania Ngao ya Jamii.
0 COMMENTS:
Post a Comment