August 29, 2017


Chelsea na Arsenal zimekubaliana kuhusiana na uhamisho wa Alex Oxlade-Chamberlain.

Chelsea imekubali kutoa pauni milioni 35 kumnasa na mambo yakienda vizuri, huenda leo akafanya vipimo.


Katika mechi iliyopita, Arsenal ilitwangwa mabao 4-0 na Liverpool huku Oxlade-Chamberlain akicheza kama beki wa kulia, jambo lililozua mjadala mkubwa kuhusiana na uamuzi huo wa Kocha Arsene Wenger kumpanga katika nafasi hiyo.

Siku chache zilizopita, Oxlade-Chamberlain alikataa kuongeza mkataba na Arsenal na mshahara wake ungekuwa pauni 180,000 kwa wiki!

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic