August 23, 2017

NYAMLANI

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Wallace Karia amewateua Makamu wa Rais wa zamani wa TFF, Athuman Nyamlani na Ahmed Mgoyi kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.

Rais Karia ameteua kwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya TFF ikiwa ni wiki moja baada ya kupatikana kwa viongozi wa shirikisho katika uchaguzi mkuu uliofanyika Agosti 12, mwaka huu.

Rais Karia aliwatambulisha viongozi hao kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji iliyofanyika Jumanne Agosti 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Nyamlani alikuwa mgombea wa urais katika uchaguzi uliomuweka madarakani Karia, lakini alijitoa mwishoni huku Mgoyi amekuwa mjumbe wa kamati kwa kipindi kirefu, naye alitangaza kujiuzulu nafasi yake hiyo kabla ya uchaguzi huo uliofanyika mjini Dodoma Agosti 12, mwaka huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic