August 22, 2017



Beki wa zamani wa Simba, Abdi Banda amesema namna ilivyo ligi ya Afrika Kusini, anaona ana nafasi ya kupata nafasi ya kupata mafanikio zaidi.

Banda ambaye anachezea Baroka FC, amesema tokea acheze mechi ya kwanza ameona kuna mengi atajifunza lakini ana nafasi ya kufanya vizuri.

“Kawaida unaona, kwamba baada ya kucheza hapa kuna kuna niji. Ligi ni ngumu na ina kasi. Lakini huku kuna nafasi nzuri ya maandalizi na uwezo wangu nilionao, ninajiamini nitafanya vizuri,” alisema.


Awali Banda ambaye alimaliza Ligi Kuu Bara msimu uliopita kwa kiwango cha juu alisema ligi ya Afrika Kusini itamtoa kwenda kucheza barani Ulaya hivyo anaitumia kama njia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic