August 20, 2017




Yanga imeendeleza ushindi katika mechi zake za kirafiki baada ya kuigonga Jamhuri ya Pemba kwa bao 1-0.

Yanga ambao walionyesha soka safi zaidi katika kipindi cha kwanza, walipata bao lao mapema kabisa katika dakika ya 5 tu.

Bao hilo, lilifungwa na beki wake wa kushoto Mwinyi Haji ambaye aling’ara katika mchezo huo.

Baada ya ushindi huo, Yanga inaonekana itakuwa tayari kwa ajili ya mechi yake ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, keshokutwa Jumatano.


Yanga inatarajia kurejea Dar es Salaam mapema kesho kwa ajili ya maandalizi ya mwaisho ya mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic