August 13, 2017

 Mkutano mkuu wa Klabui ya Simba umeshaanza muda mfupi uliopita kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyarere international Conference Centre).

Ukumbi huo wa kisasa kabisa nchini upo maeneo ya Ocean Road, jirani na Chuo cha Usimamizi wa fedha (IFM), ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kufanyia mkutano wake kwenye kituo hicho kilichobeba jina la Baba wa Taifa.

Tayari wanachama wa klabu hiyo wameshawasili na mkutano umeanza huku kukiwa na kipupwe tofauti na mikutano mingine iliyopita ambapo imekuwa ikifanyika kwenye sehemu za wazi au kweny ukumbio ambao hauna kipupwe.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV