August 13, 2017









Usain Bolt aliumia na kushindwa kumaliza mbio zake za mwisho za ubingwa wa dunia jijini London, na mwanariadha mwenzake Yohan Blake anasema huenda kucheleweshwa kwa mbio hizo kulimwathiri.

Bolt alipata mkakamao wa misuli na kulazimika kuondoka uwanjani alipokuwa akikimbia mbio za kupokezana vijiti za 4x100m ambazo timu ya Uingereza ilishinda.


Yohan Blake alisema hilo: "Mbio zilicheleweshwa dakika 10, tuliwekwa tukisubiri kwa dakika 40. Ilitushangaza sana.
"Watuweka muda mrefu sana tukisubiri."

Bolt alikuwa ametumai kwamba angemaliza maisha yake ya ukimbiaji kwa kushinda dhahabu mbili mashindano hayo ya London lakini ameondoka sasa na nishani ya shaba pekee aliyoishinda kwenye mbio za mita 100 wikendi iliyopita.

Sekunde chache baada yake kupokezwa kijiti awamu ya mwisho ya mbio hizo, alitatizima na kuanguka sakafuni.

Daktari wa timu ya Jamaica Kevin Jones amethibitisha kwamba Bolt alipatwa na mkakamao wa misuli ya mguu wake wa kushoto.
"Ilikuwa dakika 40 na walitoa nishani kwa washindi wa mbio mbili kabla yetu kukimbia," aliongeza bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 Blake.

"Tulikaa tukipasha misuli joto na kusubiri, kisha tunapasha misuli moto tena na kusubiri. Nadhani hilo lilitwathiri.

"Inauma kumuona jagina halisi, bingwa halisi akiingia uwanjani na kutatizika kwa namna hiyo."

Bingwa wa mbio za 110m za kuruka viunzi Omar McLeod, aliyeongoza timu ya Jamaica ambayo ilikuwa imeshinda ubingwa wa mbio za 4x100m katika makala manne yaliyopita ya ubingwa wa dunia, alikubaliana na mtazamo wa Blake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic