August 27, 2017



Pamoja na majigambo yake, mashabiki wa Simba waliamua kumnunulia maji Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ili kumpoza machungu.

Simba imeitwanga Ruvu Shooting kwa mabao 7-0 katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Bara ikiwa ni siku chache baada ya mwalimu huyo kitaaluma ambaye ni msemaji wa timu hiyo ya jeshi kusema Simba ni toy au mwanasesere.

Mashabiki hao waliamua kumnunulia Masau maji ya kunywa na kumpelekea kwenye gari la wachezaji wa timu ya Ruvu.

Kabla ya hapo, wengi waliamua kupiga naye picha wakimvisha kofia za Simba na wengine wakimshangilia.


Muda wote baada ya mchezo huo kwenye Uwanja wa Uhuru, Masau alionekana mtulivu na asiye na makuu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic